Wednesday, February 11, 2015

ANGALIA MAGARI YASIYOKUWA NA DEREVA HUKO UINGEREZA.

ad300
Advertisement
Serikali inataka Uingereza kutambulika ulimwenguni kama kiongozia wa teknolojia ya magari yasiokuwa na dereva.
Itachapisha sheria katika majira ya kiangazi ambayo itaruhusu majaribio ya magari hayo kuwa na uhuru wa kujiendesha.
Serikali imeahidi kuangaziwa upya sheria zilizopo ifikiapo majira ya kiangazi ya mwaka 2017.



Mpango huo utabaini iwapo kiwango cha juu cha uendeshaji magari kitahitajika miongoni mwa magari yanayojiendesha.
Pia sheria hiyo itaangazia ni nani wa kulaumiwa iwapo kutakuwa na ajali mbali na usalama wa madereva na watembeaji wa miguu.
Ripoti ya Idara ya usalama imekiri kwamba magari yanayojiendesha bila madereva huenda hayafuati maagizo na kwamba majaribio yanayoendelea yatahitaji kuwashirikisha madereva waliofuzu kuyaendesha magari hayo.


Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 Post a Comment: