Advertisement |
MANCHESTER United imeponea chupuchupu kulala mbele ya West Ham United baada ya kuata sare ya 1-1 ugenini usiku huu.
Cheikhou
Kouyate aliifungia West Ham bao la kuongoza dakika ya 49 na United
wakahaha tangu hapo kusaka bao la kusawazisha hadi kuelekea kupoteza
mchezo.
Hata hivyo, kiungo Daley Blind akawanusuru Mashetani Wekundu kulala baada ya kufunga bao la kusawazisha dakika ya 90.
Man
United ilipata pigo baada ya beki wake Luke Shaw kuonyeshwa kadi ya
pili ya njano na kuwa nyekndu. Pamoja na matokeo hayo, Man United
wanabaki nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi, wakati West Ham wanabaki
nafasi ya nane.
0 Post a Comment: