Advertisement |
Uongozi wa klabu ya Simba umetangaza mkakati wa kupata ushindi kwenye mechi zilizosalia za Ligi Kuu msimu huu wakieleza kuwa, sare sasa basi.
Mikakati hiyo itaanzia Shinyanga ambako kikosi chao kilikwenda jana tayari kuikabili Stand United, Jumamosi.
Baada ya kupanda hadi nafasi ya nne baada ya
kuishinda Polisi Morogoro mabao 2-0 Jumapili, Simba itaanza dhamira hiyo
kwa kibarua kigumu dhidi ya Stand United kwenye Uwanja wa Kambarage
mjini Shinyanga.
Rais wa Simba, Evance Aveva aliliambia gazeti hili
jana kuwa, wanatambua ugumu wa ligi ya msimu huu, lakini wa mkakati wa
ushindi katika mechi zao zilizosalia na kusisitiza kuwa hivi sasa kila
mechi kwao ni fainali.
“Uongozi tumekaa na benchi letu la ufundi pamoja
na wachezaji na kukubaliana kwa kauli moja kuwa, hakuna kufungwa.
Mkakati tuliouweka ni kuelekeza nguvu, akili na kucheza kama fainali
katika mechi zetu zote zilizosalia, hakuna kudharau mechi ili kupata
matokeo mazuri, tayari tumefanikiwa Morogoro na sasa tunaelekea
Shinyanga.
“Tunatambua ugumu wa kucheza ugenini, kama uongozi
tumeipa sapoti ya kutosha timu yetu na benchi la ufundi na timu
inakwenda Shinyanga na kauli moja tu kuwa Simba sasa matokeo ya sare au
kufungwa basi.
“Mashabiki wetu watuunge mkono na kutusapoti kwa
nguvu zote ili kushinda mchezo huo na mechi nyingine zilizosalia na
niwaambie tu timu yao sasa haitawaangusha,” alisema Aveva.
0 Post a Comment: