Advertisement |
Tuliziona pichaz Yamoto Band
pamoja na story za wao kwenda zao London, Uingereza kupiga show, siku
ya leo FEB21 muda mfupi baadaye watakuwa na show, watu wetu hawa saa
chache zilizopita walikuwa kwenye Interview na mtangazaji Charles Hillary kwenye BBC Dira ya Dunia.
Swali la kwanza kuulizwa ilikuwa wapi lilikozaliwa jina la Yamoto Band? ;”Ukiachana
na vitu vya motomoto ambavyo tunavitoa ni jina ambalo lilibeba nyimbo
yetu ya kwanza.. Yamoto Band ni zao la Mkubwa na Wanae, kituo ambacho
kinalea watoto wenye vipaji..“– Aslay.
Kuhusu ishu ya mtu anayewaandikia nyimbo zao; “Mara nyingi sana tunaandika wenyewe lakini tunashare idea na bosi wetu Mkubwa Fella.. Tunakaa naye na tunashare idea“– Aslay.
Hapa wanaongelea utofauti wa Yamoto Band na band nyingine; “Vitu
vingi vishafanyika, uongozi wetu unataka sisi tuwe wapya ndio maana
bendi unaona iko tofauti kwanza tuna umri mdogo.. nyimbo zetu zina
dakika tatu nne tofauti na bendi nyingine..“– Maromboso.
Band nyingi zinavunjika, unadhani hii itatokea kwa Yamoto?; “Sisi tumekaa ni zaidi ya miaka minne tuko pamoja kabla ya Yamoto Band
kujulikana tunajua nini maisha halafu tumetoka katika maisha magumu..
Sio rahisi leo unishawishi kwa vitu vidogo milioni mbili milioni tatu
wakati tunategemea mamilioni mengi baadaye“– Aslay.
Ni nini siri ya umoja wao?; “Tumekaa
muda mrefu sana kwenye tundu moja kwa hiyo tumeshazoeana hata tabia
zetu.. Tumeshakuwa kama ni ndugu sasa na sio marafiki tena“– Bella.
Hapa Charles aliomba kuambiwa maana ya ‘Kupwelepweta‘; “Kupwelepweta ni kitu ambacho hakikutoshi, kama mimi nivae koti lako lazima linipwelepete…“– Aslay.
0 Post a Comment: