Advertisement |
Mshambuliaji
wa klabu ya Chelsea Diego Costa amesema hajawahi kumjeruhi mchezaji
mwenzake kwa makusudi mchezoni na kwamba tuhuma hizo dhidi yake ni
changamoto anazozipitia na ataendelea kuwa imara. Mchezaji huyo raia wa
Brazil mwenye miaka 26 amemaliza kutumikia adhabu ya kutocheza mechi
tatu kutokana na kufungiwa kwa kile kilichodaiwa kumuumiza mchezaji wa
Liverpool katika mchezo wa nusu fainal mwezi jana. Costa mwenyewe
amesema kuwa kuwa hana historia ya mchezo huo mchafu wa kuweza kumuumiza
mchezaji mwenzake kwa kudhamiria.
Kocha wa Chelsea Jose Mourinho
amelalamikia hatua ya kufungiwa kwa mchezaji wake na kudai kuwa ilikuwa
ni tukio la bahati mbaya japo amevituhumu vyombo vya habari kwa kulipa
uzito mkubwa Zaidi suala hilo kuliko hali halisi.Costaaliyejiunga na Chelsea kwa paundi milioni 32 mwezi July mwakajana anasema kuwa amekuwa akichezewa vibaya zaidi na wachezaji wengine matukio yanayowastahili kuchukuliwa adhabu kali kwa makosa kama hayo lakini kwake yeye mambo yanakuwa makubwa zaidi.
0 Post a Comment: