![]() |
Advertisement |
Ivory Coast imepanda katika orodha ya shirikisho la soka duniani FIFA baada ya kushinda kombe la mataifa ya Afrika mwaka huu.
Equitorial Guinea waandalizi wa kombe hilo pia walipanda na kuorodheshwa miongoni mwa mataifa 50 bora duniani.Kikosi hicho kilipanda nafasi 69 na sasa kiko sawa na Congo katika nafasi ya 49 baada ya kufika nusu fainali ya mchuano huo ijapokuwa kwa utata.
Ndovu hao wameorodheshwa wa pili barani Afrika nyuma ya Desert Foxes,timu walioishinda katika robo fainali.
Timu ya Ghana ambayo ilicheza katika fainali ya kombe la mataifa ya Afrika dhidi ya walioibuka washindi Ivory Coast imepanda nafasi 12 hadi nambari 25.
Katika nafasi za kwanza ,Ujerumani bado inashikilia nafasi ya kwanza ikifuatiwa na Argentina,Colombia,Belgium na Uholanzi katika nafasi ya 5.
Hakuna timu mpya zilizoingia katika orodha ya mataifa kumi 10 duniani.
Mataifa kumi bora barani Afrika: 1. Algeria 2. Ivory Coast 3. Ghana 4. Tunisia 5. Cape Verde 6. Senegal 7. Nigeria 8. Guinea 9. Cameroon 10. Congo DR
Mataifa kumi bora duniani 1. Germany 2. Argentina 3. Colombia 4. Belgium 5. Netherlands 6. Brazil 7. Portugal 8. France 9. Uruguay 10. Spain
0 Post a Comment: