Advertisement |
Ushindi huo, unaifanya Azam FC ifikishe pointi 25 baada ya kucheza mechi 13, sawa na Yanga SC wanaoangukia nafasi ya pili kwa kuzidiwa wastani wa mabao.
Hadi mapumziko, tayari Azam FC walikuwa mbele kwa mabao 3-1 yaliyofungwa na mshambuliaji kutoka Ivory Coast, Kipere Tchetche, kiungo mzawa Frank Domayo na mpachika mabao wa Burundi, Didier Kavumbangu.
Wachezaji wa Azam FC wakishangilia bao lao la tano leo Chamazi |
Tchetche, mfungaji bora wa Ligi Kuu msimu miwili iliyopita, alifunga bao lake dakika ya 19 baada ya kuwahi mpira uliogonga mwamba kufuatia kipa Said Mohammed kushindwa kuokoa shuti la winga Mganda, Brian Majegwa.
Domayo akaifungia bao la pili Azam FC dakika ya 26 akimalizia pasi fupi ya Brian Majegwa ndani ya 18.
Mtibwa Sugar ikazinduka dakika ya 34 baada ya kupata bao la kwanza, lililofungwa na Mussa Nampaka kwa shuti la kushitukiza kufuatia pasi ya Ally Shomary.
Kavumbangu akaifungia bao la tatu Azam FC akimalizia pasi nzuri ya kiungo, Salum Abubakar ‘Sure Boy’.
Azam FC ilirudi na moto wake kipindi cha pili na kufanikiwa bao la pili mapema tu dakika ya 58, Frank Domayo tena akiwainua vitini mashabiki Uwanja wa Azam Complex, baada ya kuwahi mpira uliotemwa na kipa Said Mohammed.
Frank Domayo katikati ya wachezaji wa Mtibwa Sugar |
Ame Ally ‘Zungu’ akaifungia Mtibwa Sugar bao la pili dakika ya 70 baada ya kupokea pasi ya Abdallah Juma ambaye aliingia muda huo huo kuchukua nafasi ya Mussa Mgosi.
Kipre Herman Tchetche akaifungia bao la tano Azam FC dakika ya 86 akiunganisha krosi ya beki Shomary Kapombe.
Kikosi cha Azam FC kilikuwa; Aishi Manula, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni/John Bocco dk65, Said Mourad, Serge Wawa, Kipre Bolou/Mudathir Yahya dk55, Kipre Tchetche, Frank Domayo, Didier Kavumbagu/Khamis Mcha ‘Vialli’ dk80, Salum Abubakar na Brian Majwega.
Mtibwa Sugar; Said Mohammed, Andrew Vincent, Majaliwa Mbaga, Ally Lundenga, Salim Mbonde, Shaaban Nditi, Ramadhani Kichuya, Mussa Nampaka, Ame Ally, Henry Joseph/Ally Shomary dk33 na Mussa Mgosi/Abdallah Juma.
0 Post a Comment: